Arusha: Wizi wa Kura, Rushwa Wavuruga Uchaguzi wa Ndani CHADEMA, Lema Atajwa Kinara wa Migogoro makada watupiana makonde live. - Mzalendo Daily

Arusha: Wizi wa Kura, Rushwa Wavuruga Uchaguzi wa Ndani CHADEMA, Lema Atajwa Kinara wa Migogoro makada watupiana makonde live.

0
81

Wakati vyama mbalimbali vikiendelea kufanya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hali imeendelea kuwa mbaya zaidi kwa CHADEMA baada ya kutokea vurugu na kutupiana makonde hadharani jijini Arusha kwenye uchaguzi wa ndani wa mkoa wa chama hicho hapo jana Novemba 13 kwenye Ukumbi wa Golden Rose.

Uchaguzi huo ulifunguliwa na hotuba kutoka kwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Mjumbe wa Halmashauri Kuu CHADEMA na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godless Lema ambapo, wanachama wa chama hicho wanadai hotuba hiyo ilichochea vurugu hizo na pia, Bwana Lema anatajwa kama kinara wa vurugu hizo.

Wanachama hao walitupia maneno makali na hata ngumi baada ya madai kwamba uchaguzi wa mkoa uligubikwa na wizi wa kura, rushwa na upendeleo.

Moja ya mwanachama ambaye alionekana akilalamika kwa kushambuliwa na kikundi cha vijana wa hamasa wa chama hicho alisema kwamba, baadhi ya wapiga kura walisafirishwa kwa siri kutoka Loliondo na Longido kwenda Arusha kwa ajili ya kumpiga kura mgombea anayepeungwa mkono na Lema.

Mwanachama huyo anaeleza kwamba Lema ndiye aliyetoa maagizo ya yeye kushambuliwa na vijana wa hamasa baada ya kusimama kidete kutaka kuzuia wizi wa kura na dhuluma iliyotaka kufanyika kwenye uchaguzi huo.

Mwanachama huyo ambaye jina lake halikufahamika aliongeza pia kwamba, mwaka jana alishiriki uchaguzi wa ndani na wakati wa kuhesabu kura taa za ukumbi zinazimwa mara tatu hali iliyosababisha kura zake kuibiwa na hatimaye kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Ili kuzuia hali hiyo mwaka huu waliamua kwenda kununua taa za dharura endapo umeme ungekatika basi waweza kuzitumia na kuzuia wizi. Lakini baada ya kuwasili ukumbini hapo akiwa na taa hizo, alijikuta anashambuliwa kwa makonde mazito na vijana wa hamasa na kuzuiwa kuingia ukumbini.

Baada ya vurugu kali na mvutano nje ya ukumbi huo, lawama zote zilielekezwa kwa Lema na genge wakimtuhumu kuwa na mienendo inayowakatisha tamaa ndani ya chama. Wamesema kuwa mienendo hiyo imekuwa chanzo cha migogoro na kutokuelewana miongoni mwa wanachama.

Hali ilipozidi kuwa mbaya katika eneo hilo Lema alionekana kukwea gari yake na kutokomea mbali bila kuaga na kuacha mtafaruku mkubwa kwa wanachama wake. Watu walioshambuliwa na vijana wa hamasa wamesema kwamba watamfungulia Lema mashitaka na vijana aliowatuma kwa kuwajeruhi.

Leave a reply