Zitto atoa kauli tata zinazoashiria umwagaji damu/machafuko Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2025. - Mzalendo Daily

Zitto atoa kauli tata zinazoashiria umwagaji damu/machafuko Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2025.

0
111

Aliyekuwa kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiwa kwenye mahojiano ya kipindi cha Kasri kinachoongozwa na Mtangazaji Salim Kikeke kwenye kituo cha redio ya Crown fm, amesikika akisema uchaguzi mkuu ujao wa 2025 Zanzibar Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinapaswa kuwa makini sana.

Kauli hiyo ilimshtua mwongoza kipindi Salim Kikeke na kuwiwa kumuuliza Zitto “mtafanya nini”?, Zitto alishusha pumzi kidogo kisha akasema sasa hivi hakuna tena mtu kama Maalim Seif na hata 2025 hatokuwepo hivyo, Serikali inapaswa kuwa makini sana.

Kikeke alionekana kutoridhishwa na jibu hilo hivyo alimtaka Zitto achambue zaidi. Zitto aliongeza kwamba, Alikuwepo ‘Gaint’ hapo awali, yaani Maaalim Seif, mtu ambaye aliweza kuwatuliza na kuwarudisha nyumba Wazanzibar katika nyakati za tata za chaguzi zilizopita huko nyuma lakini sasa, mtu huyo hayupo tena.

Zitto alisema kwamba kuna makubaliano ambayo waliingia na serikali kabla wao kama ACT kukubali kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) mwaka 2020, makubaliano ambayo serikali ya Mh. Hussein Mwinyi inaonekana kuwa na ajizi kuyatekeleza na moja kati ya hayo ambalo la msingi zaidi, ni kuondoa utaratibu wa kupiga kura mara mbili.

Zanzibar kuna utaratibu wa kupiga kura kwa siku mbili. Siku ya kwanza kwa vyombo vya ulinzi na usalama na maafisa wa tume ya uchaguzi na siku ya pili kwa umma mzima. Hali hii ilizua taharuki kubwa sana uchaguzi mwa mwaka 2020 ambapo Chama cha ACT Wazalendo kiliiandikia barua Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kutaka ufafanuzi na kuondoa shaka juu ya kura ya mapema lakini bado majibu ya ZEC hayakutosheleza.

Zitto aliongeza kwamb Othman Masoud Othman sio Maalim hivyo wawe [Serikali] wawe makini sana. Kikeke akauliza tena “Hiyo ina maana gani”, “Hivyo hivyo”, Zitto akajibu. “Zitto utaniweka mashakani naomba ufafanue una maana gani”, Salim aliomba ufafanuzi zaidi wa kauli tata za Zitto.

Kwa sauti ya upole na yenye ‘userious’ mkubwa sana, Zitto alitoa ufafanuzi wa kuali yake kwa kusema kwamba, chama chake kinahitaji masuala yote machache sana na ya msingi sana waliyokubaliana na serikali ya Rais Mwinyi yatekelezwe. ACT na CCM kabla ya kuunda SUK 2020 kuna majambo yalipaswa kutekelezwa kama kufanya marekebisho ya sheria za uchaguzi na kusimamia uchaguzi, mambo ambayo hadi muda huu mchache uliobaki kuelekea Uchaguzi Mkuu, hayajatekelezwa.

Kauli ya Zitto inaashiria kwamba ACT Wazalendo haitokuwa na mswalie mtume kwenye uchaguzi wa 2025 endapo hawaona kuna dhuluma za wazi zimefanyika dhidi yao kwenye uchaguzi huo. Zitto pia amesema ya kwamba, kupitia mtindo wa kupiga kura mara mbili, watu 21 waliuawa kwenye uchaguzi wa 2020 na hivyo basi, hilo hawatoruhusu litokee tena 2025 na kama chama, hawatokubali kushiriki uchaguzi ambao utakuwa na upigaji kura mara mbili kwani kufanya hivyo, ni sawa na kupeleka watu wao machinjioni, aliongeza Zitto.

Comments are closed.