Mkwamo wa DEMOKRASIA ndani ya CHADEMA na mashaka juu ya uadilifu wa MBOWE. - Mzalendo Daily

Mkwamo wa DEMOKRASIA ndani ya CHADEMA na mashaka juu ya uadilifu wa MBOWE.

0
157

Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kilianzishwa mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya katiba ya Tanzania pamoja na msukumo wa ndani na nje kuhusu wimbi la demokrasia ya kiliberali ya mfumo wa vyama vingi. Waasi wa Chadema ni pamoja na Edwin Mtei,Ndesamburo,Bob Nyanga Makani, Brown Ngwilulupi na Dkt Kabourou. Kwakuwa Chama hicho kilijitanabaisha kupigania haki, utawala bora na demokrasia hivyo kiliweza kupata wapiga kura wengi vijana na hatimae kuchukua nafasi ya CUF na kuwa Chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Chadema tangu mwaka 2004 inaongozwa na Ndugu Mheshimiwa Freeman Mbowe mpaka leo hii ni takribani miaka 20 yuko madarakani kama mwenyekiti wa chama.

Mheshimiwa Mbowe ni kiongozi mwenye sifa zote za kumpima kwa ubaya na uzuri.

Unaweza kuandika kitabu chenye kurasa 100,000 kuthibitisha unazi,uhafidhina na udikteta wa Mbowe ndani ya Chadema kuanzia matumizi ya fedha za Chama, migogoro ndani ya chama na sakata la udini, ukabila na ukanda kwenye halmashauri kuu ya Chadema kupitia maamuzi ya kuteua viongozi na mambo Vivyo hivyo unaweza kuandika kitabu chenye kurasa 100,000 kuthibitisha uadilifu wa Mbowe ndani ya Chadema kwa kipindi cha miaka 20.

Mbowe ni mfano wa kiongozi aliyepigania uhuru wa nchi na kutaka kujilipa baada ya mapambano ya Uhuru yaani anakula fungate ya mapambano na jasho lake ndani ya Chadema.

Tangu mwaka 2000 wameondoka wanasiasa maarufu zaidi ya 600 Chadema na wote ukiwauliza tatizo ni uadilifu wa Mbowe. Hivi karibuni nilifanya mahojiano na aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu Chadema kuanzia mwaka 2005_2010 Ndugu Mheshimiwa Muhonga Saidi Ibrahim Ruhwanya alinieleza uhafidhina wa Mbowe ndani ya Chadema ambao umekuwa ni kikwazo kwa chama kufikia malengo yake ya kimkakati na ushawishi. Chadema ya mitandaoni ni tofauti na Chadema halisi kupitia uweledi na mikakati kwenye vikao vyao.

Kwakuwa Chadema na viongozi wake hutumia muda mwingi kuishambulia CCM na serikali yake kuanzia majukwaani na mitandaoni hivyo hutumia njia hiyo kuficha mapungufu yao ya kimfumo na utendaji ndani ya chama chao. Hakuna sehemu kwenye katiba ya Chadema inasema mwenyekiti ataongoza miaka 20.

Kitendo cha Mbowe kuamini Kwamba akistaafu uongozi ndani ya Chadema kutatokea hitilafu na tandawi hii inathibitisha Kwamba Chama kimekosa mikakati ya kuandaa warithi sahihi wa baadae kwa maslahi mapana ya Chama chao.

Mwaka 2005 zaidi ya wanasiasa 30 mkoani Kigoma waliondoka Chadema wakiongozwa na Nyamtema na wenzake kutokana na uongozi wa Chama mkoa kuingia kwenye mgogoro na makao makuu ya Chadema, yaani wanachama wa mkoa wanafanya maamuzi lakini Mbowe anapindua meza kinyume na msingi wa katiba ya Chadema yenye msisitizo wa neno sisi wanachama wa Chadema.

Mwaka 2007_2008 Hayati Chacha Zakayo Wangwe aliyekuwa mbunge wa Tarime aliingia kwenye mgogoro mzito na Mbowe kisa kuhoji maamuzi ya Mbowe ambayo mara nyingi huathiri Chama hasa kutumia kampuni ya kaka yake kununua mali za Chama kama magari na vifaa vingine kutoka nje,hata hivyo Wangwe alihoji uhalali wa Mbowe kukipangisha Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kwenye nyumba yake ya Kinondoni Makaburini mtaa wa Ufipa.

Bado Watanzania hawajasahau jinsi viongozi wa Chadema walivyowabagaza akina Zitto Kabwe na Samson Mwigamba kabla ya kuwafukuza na kutimkia Act Wazalendo.

Hivi karibuni Ulifanyika uchaguzi wa Chadema Kanda mbalimbali ambapo kwa ukanda wa Nyasa Mchungaji Peter Msigwa alilalamika ushindi wa figisu wa Joseph Mbilinyi dhidi yake.Hatimae Msigwa aliamua kuondoka Chadema na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM na kukaribishwa na Dr Samia Suluhu Hassan mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano mkuu wa halmashauri kuu ya CCM Lumumba Dar es Salaam.

Kama kawaida yao viongozi wa Chadema na wanachama wake walitumia mitandao ya kijamii kumdhihaki na kumchafua Msigwa kwa lengo la kuficha mapungufu yao na kulinda uadilifu hewa na visa bandia vya Freeman Mbowe.

Hali hii ilipelekea sintofahamu ndani ya Chadema mpaka wasomi na wanazuoni wa Afrika kama Dr Nelson Chamisa wa Zimbabwe ambaye alinipigia simu kwa njia ya Whatsapp na kuniuliza Chadema wanapata wapi uhalali wa kuishambulia CCM wakati ndani ya chama chao hakuna demokrasia?

Maswali hayo yanaibua sintofahamu na sera za Chadema kuendesha chama kwa matukio na kiki za mitandaoni bila Kuwa na sera za ushawishi kwa wapiga kura. Watanzania Wana matatizo ambayo wanahitaji majibu ya kisayansi na serikali ya Tanzania inafanya kazi usiku na mchana wakati viongozi wa Chadema kazi yao ni kupandikiza sumu,chuki na husda ili wananchi waichukie serikali yao pendwa .

Kwa hili nakiona Chama cha Demokrasia na maendeleo kupoteza ushawishi na nafasi yake kuchukuliwa na Act Wazalendo baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Watanzania wa sasa hivi wanajua mbivu na mbichi hivyo viongozi wa Chadema wanapaswa kujitafakari kuhusu migogoro ndani ya chama chao kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Na kama wakiendelea na uhafidhina Kwamba Kila anayeondoka Chadema anakuwa amenunuliwa watakuwa wanajitengenezea kifo chao cha taratibu. Ni mbumbumbu Mzungu wa reli tuu na mnazi wa Chadema ndio anaendelea kuamini Kwamba Mbowe ni msafi na muadilifu na Chadema haina tatizo lolote.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Afrobarometer mtandao wa utafiti wa Kiafrika usioegemea upande wowote unatoa mwanga kuhusu kwa nini hali hii iko hivi.

Utafiti huo, ambao ulihusisha mahojiano 9,500 yaliyofanywa mwaka 2020_2023 huko Botswana, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe, ulionyesha uungwaji mkono mkubwa kwa siasa za vyama vingi.

Lakini matokeo pia yanaonyesha kuwa vyama vya upinzani vinakabiliwa na vikwazo vikubwa kupata uungwaji mkono wa wengi. Hii ni pamoja na ukweli kwamba haviaminiki kama vyama tawala na mara nyingi havionekani kama mbadala wa kweli kwa chama tawala.

Nchi zote tano zinatawaliwa na vyama vilivyotokana na harakati za ukombozi na vimekuwa madarakani kwa miongo kadhaa tangu uhuru. Ingawa baadhi ya vyama hivi tawala vimepoteza uungwaji mkono wa wapiga kura katika miaka ya hivi karibuni, uungwaji mkono wa upinzani haujakuwa wa kutosha kuwatoa madarakani.

Suala la kuaminiwa
Matokeo ya hivi karibuni yanaakisi matokeo ya utafiti uliofanywa katika nchi 36 za Afrika mwaka 2020 ambao ulibaini kuwa vyama vya upinzani vilikuwa na viwango vya chini zaidi vya uaminifu miongoni mwa aina 12 za taasisi na viongozi. Wakati uaminifu kwa vyama tawala ulikuwa ni asilimia 46%, na asilimia 20% tu kwa vyama vya upinzani.

Hii ilikuwa ni maboresho ikilinganishwa na hali iliyokuwepo zaidi ya muongo mmoja uliopita ambapo viwango vya uaminifu kwa vyama vya upinzani vilikuwa vya chini zaidi.

Kupinga mageuzi ndani ya Chadema na kukandamiza wakosoaji ndani ya Chadema ni kuhujumu demokrasia. Mheshimiwa Mbowe ni muhujumu namba moja wa demokrasia nchini Tanzania kwa sababu yale anayohubiri jukwaani ni tofauti na yale anayofanya na kuwafanyia wengine ndani ya Chadema ambapo amekifanya chama hicho kama mali yake binafsi.

Leave a reply