Kilichotokea Kenya si Demokrasia, ni Demoghasia. - Mzalendo Daily

Kilichotokea Kenya si Demokrasia, ni Demoghasia.

0
103

Demokrasia ni serikali ya watu kwa ajili ya watu. Kanuni zake za msingi ni utawala wa sheria na mgawanyo wa madaraka. Chini ya mfumo wa kidemokrasia, utawala wa sheria unatawala uendeshaji wa serikali na Bunge, na unawapa majaji uwezo wa kuthibitisha kama utawala umefuata sheria hiyo.

Ni jukumu la mfumo wa kidemokrasia kupima daraja sahihi kati ya hatua madhubuti za serikali na utawala, na ulinzi wa haki na uhuru wa raia. Hasa, mfumo lazima uweze kudumisha usawa kati ya mahitaji ya maslahi ya jumla ya jamii na yale ya ulinzi wa haki za msingi za kila mtu kama ilivyowekwa katika Mkataba wa Ulaya wa Haki za Binadamu. Hii inajumuisha kuheshimu haki za walio wachache na walio wengi. Kando na ulinzi wa haki za kiraia na kisiasa, tahadhari inapaswa kuchukuliwa kuhakikisha kwamba raia wanapata manufaa kamili ya haki zao za msingi za kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Njia yenye mawazo mapana inapaswa pia kuchukuliwa kwa vifungu vipya vinavyotoa ulinzi kamili wa haki za binadamu.

Katika hali ya mgogoro au hali ya hatari, njia zote zinazopatikana chini ya sheria ya kawaida zinapaswa kutumiwa kabla ya kuchukua hatua za kipekee. Ikiwa suluhisho hili kali litahitajika, linapaswa kutumika tu kwa kiwango kinachohitajika na hali hiyo. Kamwe, “kiini kigumu” cha haki za binadamu hakipaswi kuathiriwa. Ikiwezekana, haki hizi zinapaswa kuzidi haki za pekee zilizolindwa na Kifungu cha 15 cha Mkataba wa Ulaya wa Haki za Binadamu.

Wiki mbili zilizopita wananchi wa Kenya walianzisha maandamano kufuatia serikali ya Kenya pamoja na Bunge kupitisha muswaada wa fedha wenye ongezeko la kodi kwa zaidi ya asilimia sitini hivyo kuifanya serikali ya Kenya kupata kiasi la Dola billion mbili ili kupunguza deni la taifa ambalo limepanda kwa zaidi ya asilimia 45 kufuatia mikopo yenye riba kubwa na ongezeko la miradi mbalimbali ya maendeleo.

Vijana wa kizazi cha miaka ya 2000 kwa kimombo Generation Z walitumia mitandao ya kijamii kama X , Instagram na Facebook kupenyeza ajenda za maandamano.

Kwa mujibu wa Makala ya jana tarehe 27/6/2024 kutoka redio ya Kimataifa ya Ufaransa RFI International.

“Polisi wa Kenya wamefyatua gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira siku ya Alhamisi kwa makundi madogo ya waandamanaji waliokusanyika tena katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, siku mbili baada ya ghasia mbaya zilizosababisha Rais William Ruto kuondoa mpango wake wa bajeti unaopingwa.

Maafisa wa polisi mnamo Juni 27, 2024 jijini Nairobi walimkamata mwanamume mmoja wakati wa maandamano kufuatia vifo vya takriban watu 25 waliokuwa wakiandamana kupinga mswada wa fedha, Nairobi, Kenya.

Makabiliano machache yalizuka mchana kati ya polisi, waliosambazwa kwa wingi katika mitaa ya katikati mwa jiji la mji mkuu, na waandamanaji waliomba haswa “Ruto lazima aondoke”. Maandamano haya mapya yaliendelea kuzua mgawanyiko mwanzoni mwa alasiri na kipaumbele kidogo kuliko kile cha Jumanne, wakati maelfu ya waandamanaji waliwasukuma nyuma polisi katika eneo la majengo ya serikali ya Nairobi.

Siku ya Alhamisi, watu wachache waliwarushia mawe maafisa wa polisi, ambao walijibu kwa mabomu ya machozi na risasi za mpira, na takriban watu saba walikamatwa, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wamebaini. Polisi wakiwa na zana za kutuliza ghasia walifunga njia za kuelekea State House – ikulu ya rais – na Bunge siku ya Alhamisi.

Maandamano pia yalifanyika katika ngome za upinzani za Mombasa (mashariki) na Kisumu (magharibi).

Siku ya Jumanne, baada ya siku za kwanza za maandamano ya amani ya kutaka kuondolewa kwa ushuru mpya uliopangwa na Bw. Ruto katika rasimu yake ya bajeti ya mwaka 2024-2025, maandamano ya Nairobi yaligeuka umwagaji damu, haswa karibu na Bunge, pamoja na baadhi ya majengo kuchomwa moto na mali kadhaa kuporwa.

Kulingana na mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali, polisi walifyatua risasi za moto kujaribu kuzuia umati huo ambao waliondoa vizuizi vya usalama na kuingia ndani ya majengo ya Baraza la Wawakilishi na Bunge la Seneti, shambulio ambalo halijawahi kutokea katika historia ya nchi hiyo huru tangu mwaka 1963. Jumla ya watu 22 waliuawa mchana, wakiwemo 19 jijini Nairobi, na zaidi ya 600 kujeruhiwa, ilisema Tume ya haki za binadamu la Kenya (KNHRC).

“Eneo lisilojulikana”

Rais Ruto alitangaza kuondolewa kwa bajeti iliyopendekezwa siku iliyofuata, lakini hii haikuwazuia waandamanaji kuendelea kuandamana siku ya Alhamisi. Zaidi ya rasimu ya bajeti, vuguvugu la maandamano limebadilika na kuwa kukashifu kwa mapana sera ya William Ruto, aliyechaguliwa mnamo mwaka 2022 kwa ahadi ya kukuza uchumi na kuinua maisha ya raia wenye maisha duni.

Alhamisi asubuhi, katika kituo cha biashara cha mji mkuu, ambapo maduka mengi yaliendelea kufungwa, Moe, aliyeajiriwa katika kiwanda cha manukato, alikuwa ameshusha pazia. “Kwa nini walilazimika kuwaua vijana hawa? Mswada huu haufai watu kufa (…) Watu wengine wana hasira na wanaweza kutaka kulipiza kisasi,” analalamika mbele ya duka lake la manukato, na kuongeza: “Tuko katika eneo lisilojulikana. .”

Siku ya Jumatano, mwanaharakati wa vuguvugu la maandamano, mwandishi wa habari na mwanaharakati Hanifa Adan, alitoa wito wa maandamano tena siku ya Alhamisi wakati wa maandamano ya “amani” ya kuwakumbuka wahanga. Saa chache baadaye, William Ruto, ambaye siku iliyopita alikuwa amesema anataka kukandamiza kwa uthabiti “vurugu na machafuko”, hatimaye alitangaza kuondolewa kwa rasimu ya bajeti, na akasema anataka mashauriano ya kitaifa na vijana.

Tangazo lililofafanuliwa mara moja na Hanifa Adan kama “operesheni ya com”, na kupokelewa kwa kutiliwa shaka na waandamanaji kadhaa, kama vile Lucky, 27, aliyekuwa katikati mwa jiji la Nairobi tangu saa 3:00 asubuhi na ambaye anahakikisha kwamba “hamwamini Ruto , hii sheria itapita kwa njia moja au nyingine.”

Deni la umma la nchi linafikia karibu shilingi bilioni 10,000 (euro bilioni 71), au karibu 70% ya Pato la Taifa. Bajeti ya mwaka 2024-2025 ilitoa shilingi bilioni 4,000 (euro bilioni 29) katika matumizi, ikiwa ni rekodi.

Waandamaji hao vijana wenye kiu ya kuiwajibisha serikali ya Kenya chini ya Dr William Ruto kuondoa muswaada wa fedha na tozo ambao umepelekea kupanda kwa gharama za maisha ikiwemo bei ghari ya chakula na bidhaa mbalimbali kutoka nje.

Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Kenya vimetumia njia za vurugu kuzima vurugu. Waandamaji waliingia bungeni na kufanya uhalifu na uhalibifu kinyume na misingi ya demokrasia, uzalendo na uadilifu kwa taifa lao.

Kinachoendelea Kenya sio demokrasia bali ni demoghasia ambapo vijana wamekosa uzalendo, uadilifu, Umoja na mshikamano kwa taifa lao.

Misingi ya demokrasia katika taifa lolote ni kutumia njia za amani, Umoja na mshikamano kudai haki. Haki ikidaiwa kwa njia za uhalifu tafsiri yake ni mbaya hata kama Nia na dhamira ilikuwa njema.

Vijana wa Kenya walipaswa kuandika makala nyingi kupitia vyombo vya habari kupinga muswaada huo,pia kuandika barua za wazi kwa Raisi na Spika wa Bunge la Kenya kuukataa muswaa huo wa fedha. Na wangetoa siku 21 za serikali kuondoa muswaada huo.

Mwisho kabisa vijana wa Kenya wangeandika barua za wazi na machapisho ya kitaaluma kwa Umoja wa Mataifa, Jumuia ya Ulaya na Marekani kuelezea athari za Sheria ya kodi.

Mbinu zinazotumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama wa Kenya kudhibiti maandamano na uhalibifu wa mali za Kenya zinafanana na mbinu zinazotumiwa na waandamaji. Wote wametumia vurugu.

Vyombo vya ulinzi na usalama vimekula kiapo cha utii kwa maslahi mapana ya Kenya. Kama serikali ikishindwa kudhibiti uhalifu na uhalibifu wa waandamaji itakuwa ni miongoni mwa serikali zilizofeli duniani yaani fragile State.

Kwakuwa waandamaji walikosa uongozi wenye busara na hekima ndio maana kinachoendelea Kenya sio demokrasia bali ni demoghasia kwa lengo la kuhalalisha vurugu na uasi kwa muktadha haramu na batili katika mchakato wa kudai haki.

Mwaka 1812 Juha mmoja nchini Uingereza Generali wa Mchongo Ned Ludd aliwajaza unga wa ndele vijana wa Uingereza kuchukia viwanda vya kisasa na mashine katika miji ya Leicester, Midland, Yorkshire, Cheshire, Lancaster na Kent. Vijana hao walivamia na kuchoma moto viwanda zaidi ya 40 kutoka mwaka 1811 mpaka mwaka 1816 kabla ya serikali ya Uingereza kuua vijana wa Ned Ludd na kumuua kiongozi wao.

Misingi ya kikatiba na Kidemokrasia katika kudai haki Iko wazi na wavuja jasho na makundi mbalimbali ambayo yanaona au kuhisi kuonewa na serikali lazima wafuate utaratibu kuepuka siasa za umwagaji damu.

Zaidi ya watu 600 Kenya wamejeruhiwa kutoka majimbo zaidi ya 30 huku 25 wakiripotiwa kufa. Kiongozi yeyote au mwanaharakati yeyote anayetafuta madaraka au uongozi kwa misingi ya vurugu, uasi, ukanda, udini na ukabila tunapaswa kumpuuza na kumbagaza hadharani.

Leave a reply